TAARIFA ZAIDI
Dira
Dira ya chama ni kuwa chombo imara cha kutetea haki za madereva wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu ambao ni wamiliki kibiashara na kuhamasisha na kutetea haki za abiria.
Dhima
Dhima ya Chama ni kuwaunganisha wanachama katika kuweka mazingira bora ya biashara na kutetea haki na maslahi na kuhakikisha wanapata elimu katika tasnia ya usafirishaji abiria
Lugha rasmi ya chama
Lugha rasmi katika shughuli za Chama itakuwa ni Kiswahili/Kiingereza.
Kauli mbiu
Bodaboda usafiri salama / bodaboda kazi kama kazi nyingine, usichukulie poa
MADHUMUNI MAKUU YA UMOJA
- Kulinda haki, wajibu na maslahi ya dereva, mmiliki ambaye ni dereva
- Kusimamia, kuendeleza na kulinda maslahi ya Watumiaji wa Pikipiki ndani ya wilaya na watendaji wa UBOJA] katika mamlaka husika za Serikali na Umma kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa kuna vivutio vya kutosha na mazingira mazuri ya kufanya biashara ya usafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki za magurudumu mawili na matatu.
- Kuhakikisha madereva wote wa pikipiki za abiria kibiashara wanafuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
- Kuwa mdau mkubwa wa usalama barabarani katika kuhakikisha jitahada za serikal! Kupunguza au kumaliza ajali za barabarani zinakuwa na mafanikio chanya kwa kushiriki katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara.
- Kuwakutanisha madereva wa pikipiki na madereva ambao ni wamiliki kibiashara ili kujadili maendeleo na matatizo yao katika matumizi ya Barabara na utoaji wa huduma zao na kutafuta mbinu ya kuzitatua changamoto za kisheria kwa kushirikiana na wasimaizi wa sheria.
- Kujadili na kushauriana na wakuu wa mamlaka zinazosimainia kanuni na sheria ya matumizi ya barabara kwa niaba ya madereva wa pikipiki na madereva ambao ni wamiliki kibiashara kufuatilia haki, maslahi na haki nyingine zinazohusiana na mazingira ya utoaji wa huduma ya usafiri wa Pikipiki ndani ya Wilaya ya Arusha.
- Kuishauri Serikali juu ya mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya utoaji wa huduma hii ya usafiri wa Pikipiki za biashara kama vile kuweka utaratibu wa maegesho, uongozi katika maengesho na serikali za mitaa
-
Kusaidiana katika shida mbalimbali ambazo zitakuwa ndani ya uwezo wa wanaumoja.
- Ugonjwa wa mwanachama, Mke pamoja na Watoto wanne (4) tu
- Msiba wa mwanachama, Baba, Mama, Mke na Watoto wanne.
- Kusaidia watoto Yatima na wasiojiweza.
- Kutembelea wagonjwa hospitalini pamoja na kuchangia kutoa damu.
-
Kudumisha amani, umoja na mshikamano katika umoja wetu pamoja na nje ya umoja. Kuomba tenda
mbalimbali katika jiji la Arusha. Kuanzisha taasisi ya mikopo kwa wana Umoja kwa ajili ya kukopeshana.
Kujadiliana na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kwa ajili ya kuinua uwezo wa kiuchumi kwa
Wanaumoja ili kupata mikopo mbalimbali kama:
- Pikipiki
- Vipuri
- Fedha
- Viwanja
- Nyumba ....nk